info@sautikwaya.co.tz Kuimarisha Kwaya Zetu, Kuendeleza Ibada Yetu

MASWALI YA KAWAIDA

Majibu rahisi.
Mwanzo mzuri.

Pata maelezo kuhusu Sauti Kwaya na namna ya kuanza kutumia huduma zake.

Maswali 10

Sauti Kwaya ni nini?+

Sauti Kwaya ni jukwaa la kidijitali la Utume wa Uimbaji na Maisha ya Kiroho. Linakusanya nyimbo, nota, Biblia, sala na huduma za jumuiya katika sehemu moja.

Ni kwa wanakwaya pekee?+

Hapana. Linawahusu waimbaji, watunzi, kwaya na kila mtu anayependa nyimbo za imani na anayetafuta huduma zinazosaidia maisha ya kiroho.

Ninawezaje kuanza kutumia?+

Bonyeza “Fungua app” ili kufungua app.sautikwaya.co.tz. Unaweza kuchagua huduma unayotaka na kuingia kwenye akaunti kwa shughuli zinazohitaji usajili.

Ninaweza kutumia kwenye simu na computer?+

Ndiyo. Fungua app.sautikwaya.co.tz kupitia kivinjari kwenye simu au computer.

Nota Plus ina nini?+

Ina nota za nyimbo, maneno na sauti zinazopatikana kwa wimbo, pamoja na makundi ya nyimbo na Nyimbo za Mwaka wa Kanisa.

Nyimbo za Mwaka wa Kanisa hupangwa vipi?+

Sehemu hii inalenga Dominika ya sasa na mbili zinazofuata, pamoja na maandalizi ya maadhimisho maalumu kama Noeli na Juma Kuu.

Huduma za maisha ya kiroho ni zipi?+

Biblia ya Kiswahili, Masomo ya Leo, Chumba cha Sala na Sauti Kwaya Bible Stories ni sehemu ya huduma za maisha ya kiroho.

Ninaweza kushiriki mawazo yangu?+

Ndiyo. Sauti Chat ni nafasi ya mijadala na mawazo ya kujenga. Fungua app na uingie kwenye akaunti ili kushiriki.

Ninatoa wapi taarifa ya hitilafu?+

Tumia ukurasa wa Mawasiliano. Tueleze huduma uliyofungua, hatua ulizofuata na ujumbe ulioonekana. Usitume nywila au namba za siri.

Ninawezaje kuwasiliana kuhusu ushirikiano?+

Tumia ukurasa wa Mawasiliano, chagua “Ushirikiano” na utueleze wazo lako. Unaweza pia kutupigia +255 763 195 559.

KARIBU NYUMBANI

Safari yako inaanza hapa.

Gundua nyimbo, Neno na jumuiya katika Sauti Kwaya.

Fungua Sauti Kwaya